Hatimaye rapper Ludacris amemchumbia girlfriend wake wa miaka minne, Eudoxie Fabiola Agnan.
Kufanya hivyo, rapper huyo alichukua ndege binafsi hadi Costa Rica
akiwa na watu wake wa karibu akiwemo binamu yake Monica na mumewe
Shannon Brown.
Wakati ndege hiyo ipo juu ya uwanja wa mkubwa, Eudoxie aliangalia
chini na kuona maneno: Eudoxie, Will You Marry Me”yaliyokuwa yamechorwa
kwenye majani.
Eudoxie alizaliwa nchini Gabon kwenye familia ya kawaida na mama
aitwaye Jermaine Agnan. Alihamia Marekani mwaka 2001 akiwa na miaka 15.
Eudoxie akiwa na mama yake enzi za utoto