Suarez alimalizia kwa haraka mpira uliotemwa na Golikipa Gianluigi Buffon kutokana na shuti kali la Lionel Messi na kuandika goli la pili kwa Barcelona.
Suarez akishangilia goli lake
Wachezaji wa Barcelona wakijiandaa kwenda kushangilia goli la kwanza la Ivan Rakitic
Andrea Pirlo na Paul Pogba waliishia kumtazama kwa macho Rakitic’ akimuadhibu Gianluigi Buffon
Rakitic ni moja ya mashujaa leo
Neymar alifunga goli la tatu na kuipa Barcelona taji la nne la Uefa ndani ya muongo mmoja, lakini huku nyuma waliwahi kubeba mara moja.
Neymar akishangilia baada ya kipyenga cha mwisho
Goli kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen akilala bila mafanikio baada ya kufungwa goli na Morata, kufuatia kuutema mpira uliotokana na shuti kali la Carlos Tevez.
Gerard Pique, Carlos Tevez, Dani Alves, Jordi Alba , Pirlo na Rakitic walibaki midomo wazi wakati, Mhispania huyo akiandika goli la kusawazisha
Morata, ambaye alifunga pia dhidi ya Real Madrid katika mechi zote mbili za nusu fainali aliendelea kuwa moto wa kuotea mbali
Rakitic na Neymar wakishangilia goli la kwanza
Rakitic, Neymar, Andres Iniesta na Lionel Messi wakishangilia goli la kwanza
Rakitic akizingirwa na wenzake baada ya kufunga goli
No comments:
Post a Comment