Wakati vita ya usajili ikizidi kupamba moto, timu ya ‘Wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City imekana kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga raia wa Uganda Hamisi Kiiza ‘Diego’.
Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amekanusha taarifa hizo akidai kwamba, hakuna jambo kama hilo na pindi jambo lolote linapokuwa limekamilika au kutokea kwenye klabu yao kuna utaratibu maalumu wa kutoa habari ili kuwafikia wanachama, wapenzi na mashabiki wa Mbeya City popote pale walipo.
“Kawasabu ni taarifa ambazo zimeenea acha zienee, kwasababu huwezi kuwazuia watu kueneza maneno au tetesi. Laini sisi pale jambo linapokuwa limekamilika moja kwa moja unaliona kupitia Mbeya City FC.com, kwahioyo kama taarifa kwetu bado haijatoka ni wazi jambo hilo kwetu halipo”, amesema Ten.
“Siwezi kulizungumzia sana jambo la Kiiza, lakini kuna vitu viwili kwenye jambo linapokuwa limekamilika taarifa inatolewa, lionaposhindikana taarifa inatolewa pia kwahiyo tusubiri tuone lipi litatokea kwasababu hiki ni kipindi cha usajili chochote kinaweza kutokea, inaweza kuwa A au B na yote yanaweza kuwa majibu”, Ten alifafanua.
”Kuhusu suala la wachezaji wa Mbeya City kuendelea kusajiliwa kwenda kujiunga na vilabu vingine vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara Ten amesema; “ni kawaida kwenye soka wachezaji kuhama kutoka timu moja kwenda timu nyingine ndiyo maana hata sisi tumechukua wachezaji wengine kutoka timu nyingine kuja kwetu ni kawaida. Kwahiyo hili jambo wala lisiwashitue mashabiki wa Mbeya City popote walipo waamini timu yao itakuwa tena kwenye sehemu ya timu mbili za juu” alimaliza Ten.
No comments:
Post a Comment