Monday, 8 June 2015

Ommy Dimpoz Amwanika Mpenzi wake Hadharani...Aweka Picha Mtandaoni na Kuitoa muda Huo Huo...ila Tumeidaka

Ommy dimpoz hatimae amemweka ubavu wake hadharani kupitia mtandao wa twitter.nakuta mka maneno yafuatayo.Am in lov with Coco.Nakuondoa haraka hiyo post

Chriss Brown Amwomba Msamaha Karrueche Walipokutana Klabu...Karrueche Amlia Bati na Kumpita Kama Hamjui

Chriss Akiomba Msamaha huku Karrueche Akiwa Busy na SimuMAPENZI yanaumiza! Hii ni baada ya staa wa muziki wa RnB, Chris Brown, mwishoni mwa wiki iliyopita kunaswa akiomba kumrudia ex-girlfriend ambaye ni modo na mtangazaji, Karrueche Tran.

Chriss na Karrueche waliachana hivi karibuni kufuatia staa huyo wa Kibao cha Royal kutomjulisha mpenzi wake huyo kuwa ana mtoto aitwaye, Royalty, mwenye umri wa miezi tisa.Karrueche alionekana kuumizwa na tukio hilo na kufikia hatua ya kusema hataki kutumiwa ‘sms’ wala kupigiwa simu na Chris.

Staa huyo alifanya jaribio la kutaka kurudiana na Karrueche usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, lakini ilishindikana. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye mitandao mbalimbali ya burudani, Chris alianza kumfuatilia ex wake huyo usiku kwenye Klabu ya Playboy huko Chicago ambapo alichukua siti ya VIP iliyo jirani na Karrueche ili iwe rahisi kuonana naye.

Lakini hata hivyo mbinu yake hiyo iligonga mwamba baada ya Karrueche kuamua kuondoka na kushuhudia Chris akimfuatilia kwa nyuma hadi nje ya klabu kabla ya kuonekana akikunja mikono mithili ya mtu anayeomba msamaha mbele ya ex wake huyo.

Mara baada ya Karrueche kuingia kwenye gari yake, Chris alijaribu kutaka kumfuata lakini alizuiwa na marafiki wa modo huyo, ndipo baba Royalty akaamua kulifuata gari lake na kuanza kumfuata kwa nyuma hadi nyumbani.Alipofika akakuta mlango umefungwa ndipo akaanza kupiga kelele sambamba na rafiki zake aliokuwa nao akitaka afunguliwe, hapo tayari ilikuwa usiku mkubwa.

Kuona hivyo Karrueche aliamua kuondoka na kwenda mgahawani ili kuondokana na kero ya kelele lakini Chris alimfuata na huko kabla ya kusikika majibizano baina yao, muda kidogo modo huyo akaonekana akiondoka eneo hilo akiwa peke yake na kuelekea nyumbani kwake.

WAGOMBEA URAISI CCM WAUKACHA MDAHALO

Si jambo geni lililotokea leo. Si jambo la kustaajabisha wagombea watarajiwa wa CCM kukimbia midahalo. Mafuruki pole,hujaijua CCM. CCM haina watu wenye hoja za haja za moja kwa moja-live arguments. CCM haina wajibu maswali ya moja kwa moja-live response.

CCM imejaa watumia fedha kushinda uchaguzini. Kuwaweka kwenye mdahalo wanachama wa CCM ni kutaka kuwadhalilisha na kuwaaibisha. Ni kutaka kuwavua nguo mbele ya halaiki. Pole Mafuruki. CCM is not reachable,try again later.

Labda kungekuwa na vyombo vya dola pembeni,wanaCCM wangetoa pointi. Wangetema cheche. Kiufupi,sisi ni waeupe na watupu kwenye midahalo. Hata Katibu Mkuu wa zamani wa CCM,Yusuf Makamba aliona hilo. Akapiga marufuku kushiriki midahalo. Mafuruki ulikuwa hujui? Pole.

CCM inabebwa na ujinga na umaskini wa watanzania. Ushindi kwanza,hoja baadaye.Aibu kukimbia,heshima imelindwa lakini. Hiyo ndiyo CCM!

MEMBE: Nikiwa Raisi wasanii wataenda Nje kujifunza...

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha anasimamia haki za wasanii ipasavyo.
Membe alitoa kauli hiyo mkoani Lindi wakati akitangaza nia ya kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

“Nitahakikisha naweka mipango imara katika kusimamia kazi za wasanii wote kunufaika na hakimiliki zao,” alisema.
Pia alisema atahakikisha wasanii wanakwenda kujifunza nje ya nchi masuala ya sanaa ili sekta hiyo ipate mabadiliko ya kimaendeleo kwa wasanii na Serikali kwa ujumla.

“Nikichaguliwa kuwa rais, nimejiwekea mikakati mingi kuhakikisha sekta ya sanaa inapiga hatua kutoka hapa tulipo sasa,” alisema Membe.
Katika mkutano huo, waliohudhuria ni baadhi ya wasanii akiwemo mchekeshaji, Adam Melele ‘Swebe’, Hemed Malyaga ‘Mkwere Orijino’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Wema Sepetu na Aunty Ezekiel ni washkaji kama kawaida.

Mastaa wa filamu za Tanzania Wema Sepetu na Aunty Ezekiel waliripotiwa kutofautiana hivi karibuni baada ya Aunty kumualika Kajala kwenye Baby Shower yake huku akijua Kajala hana maelewano na Wema Sepetu, Wema na Aunty wamewaonyesha mashabiki zao kuwa hawana tofauti tena kwa kushare picha wakiwa pamoja kama marafiki.

 

Sunday, 7 June 2015

Shilole Amsamehe Rose aliyesema anaujauzito wa Nuh Mziwanda.

Baada ya ugomvi uliotokea kati ya Shilole na video queen maarufu Rose kuhusu kauli ya Rose kuwa anaujauzito wa Nuh Mziwanda, na kwmba alikuwa naye kimapenzi mjini Morogoro, Rose amemiomba msamaha Shilole kwa kauli hio na kusema alisema akiwa na hasira sana sababu ya kipigo na kudhalilishwa na Shilole.

Jibu la Shilole, ‘Usifanye hivyo tena kwangu au kwa mwanamke yeyote‘

TAZAMA PICHA 14 KALI KUTOKA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE BARCELONA WAKISHINDA 3-1 DHIDI YA JUVENTUS


Suarez alimalizia kwa haraka mpira uliotemwa na Golikipa Gianluigi Buffon kutokana na shuti kali la Lionel Messi na kuandika goli la pili kwa Barcelona. 

Suarez akishangilia goli lake 

 Wachezaji wa Barcelona  wakijiandaa kwenda kushangilia goli la kwanza la  Ivan Rakitic 

 Andrea Pirlo na Paul Pogba waliishia kumtazama kwa macho Rakitic’ akimuadhibu Gianluigi Buffon

 Rakitic ni moja ya mashujaa leo

 Neymar alifunga goli la tatu na kuipa Barcelona taji la nne la Uefa ndani ya muongo mmoja, lakini huku nyuma waliwahi kubeba mara moja. 

 Neymar akishangilia baada ya kipyenga cha mwisho 

 Goli kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen  akilala bila mafanikio baada ya kufungwa goli na Morata, kufuatia kuutema mpira uliotokana na shuti kali la  Carlos Tevez.

Gerard Pique, Carlos Tevez, Dani Alves, Jordi Alba , Pirlo na  Rakitic walibaki midomo wazi wakati, Mhispania huyo akiandika goli la kusawazisha

Morata, ambaye alifunga pia dhidi ya  Real Madrid katika mechi zote mbili za nusu fainali aliendelea kuwa moto wa kuotea mbali

 Rakitic na Neymar wakishangilia goli la kwanza

Rakitic, Neymar, Andres Iniesta na Lionel Messi wakishangilia goli la kwanza

Rakitic  akizingirwa na wenzake baada ya kufunga goli 


Uchaguzi wa Coastal Union, Wagombea waanza kujitosa kuwania

Ikiwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi kwenye klabu ya Coastal Union unazidi kupamba moto, mgombea wa nafasi ya uenyekiti Twaha Ahmed ametangaza sababu zilizopelekea yeye kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Ahmed amesema ameamua kujitosa kwenye nafasi hiyo ili kuhakikisha klabu ya Coastal Union inapata maendeleo na kuondokana na changamoto zinazoikabili klabu hiyo.

“Nimeamua kuingia kugombea kama mwenyekiti ili kuendeleza Tanga yetu na michezo ipo ndani ya moyo wangu. Kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nikishirikiana na wadau wengine naamini tunaweza kuongoza”, amesema Ahmed.

“Coastal hakuna mpasuko ila kuna changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi, kinachotakiwa kama kiongozi ni kufanya kazi na wenzako ili kujua changamoto zilizopo na jinsi ya kukabiliana nazo pamoja na mafanikio yaliyopo na jinsi ya kuyaendeleza zaidi”, Ahmed ameongeza.

“Siwezi kusema chochote kuhusu upande wa wapinzani wangu, kila mmoja ana fursa ya kugombania nafasi yoyote, ni wewe tu unatakiwa ujieleze mipango yako ikoje. Lakini kila mmoja ana mwelekeo wake wa kiuongozi”, alimaliza Ahmed.

Twaha Ahmed anawania nafasi ya uenyekiti katika kikosi cha Coastal Union kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi Julai mwaka huu ikiwa ni agizo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutokea mgogoro wa kiuongozi kunako klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.

MBEYA CITY YAKANUSHA KUMSAJILI KIIZA

Wakati vita ya usajili ikizidi kupamba moto, timu ya ‘Wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City imekana kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga raia wa Uganda Hamisi Kiiza ‘Diego’.

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amekanusha taarifa hizo akidai kwamba, hakuna jambo kama hilo na pindi jambo lolote linapokuwa limekamilika au kutokea kwenye klabu yao kuna utaratibu maalumu wa kutoa habari ili kuwafikia wanachama, wapenzi na mashabiki wa Mbeya City popote pale walipo.

“Kawasabu ni taarifa ambazo zimeenea acha zienee, kwasababu huwezi kuwazuia watu kueneza maneno au tetesi. Laini sisi pale jambo linapokuwa limekamilika moja kwa moja unaliona kupitia Mbeya City FC.com, kwahioyo kama taarifa kwetu bado haijatoka ni wazi jambo hilo kwetu halipo”, amesema Ten.

“Siwezi kulizungumzia sana jambo la Kiiza, lakini kuna vitu viwili kwenye jambo linapokuwa limekamilika taarifa inatolewa, lionaposhindikana taarifa inatolewa pia kwahiyo tusubiri tuone lipi litatokea kwasababu hiki ni kipindi cha usajili chochote kinaweza kutokea, inaweza kuwa A au B na yote yanaweza kuwa majibu”, Ten alifafanua.

”Kuhusu suala la wachezaji wa Mbeya City kuendelea kusajiliwa kwenda kujiunga na vilabu vingine vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara Ten amesema; “ni kawaida kwenye soka wachezaji kuhama kutoka timu moja kwenda timu nyingine ndiyo maana hata sisi tumechukua wachezaji wengine kutoka timu nyingine kuja kwetu ni kawaida.  Kwahiyo hili jambo wala lisiwashitue mashabiki wa Mbeya City popote walipo waamini  timu yao itakuwa tena kwenye sehemu ya timu mbili za juu” alimaliza Ten.

INTER MILAN YAMTAKA MCHEZAJI HUYU WA MANCHESTER UNITED

Ni muda wa usajili nani anaenda wapi nani ana saini upya. Hii ni habari mpya ambayo inamhusu star Manchester united ambae anatakiwa na Inter Milan. 

Klabu ya Inter Milan inafanya juhudi ya kupata sign ya mchezaji Luis Nani ambae ni mchezaji wa Manchester united aliyekua Sporting Lisbon. Msimu huu wakati unakaribia kuisha Nani alisema hataki tena kucheza Sporting msimu ujao.

Baada ya kauli hiyo Inter Milan imetumia nafasi hiyo na matakwa ya Nani kumleta Inter Milan.

DINA MARIOS WA CLOUDS FM AFUNGUKA BAADA YA KUPIGWA BENCHI

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Mtangazaji Dina Marious Amefunga Mengi kuhusa hali yake na nini kinaendelea kwenye Ajira yake baada ya muda mrefu kuwa kimya:
Ameandika H aya:
'Katika haya maisha hamna kitu kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu ambaye hana hatia.Kwa kutumia cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo ukiamini huyo mtu hana uwezo wa kukufanya lolote
Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana na simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu.
Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa karibu.Ambae revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe kisaikolojia siku hadi siku.
Mbaya zaidi sikustahili miaka yote nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa ngazi zoote.
Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa mawazo.Na hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu kifuani kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa nimetendewa haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa sanaa tena katika kipindi kibaya sana.
All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila huruma huku wakinichekea.
Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki??
Mimi bado ni muajiriwa na ninalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu.
Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna ugomvi.
Na malizia kwa kusema sipo radio wala sipo tv kwa sasa.Maswali mnaniuliza kila siku na nina wajibu kila mara na leo nimewajibu tena.
ila nitakuwa kwa radio na tv hapo baadae acha niuze mafuta ya nazi.Maelezo ya mwanzo yamejitosheleza sanaa na sitaenda mbalii sanaa labda nikiandike kitabu ndio yatatimia.
Nimeandika haya kwa ufupi mjue hata sisi pamoja na majina tuliyonayo changamoto zipo na tunakabiliana nazo.Na ipo siku tutashinda maana mtetezi wetu yu hai ' Dina Marious

ALI KIBA AWAONESHA MASHABIKI PICHA ZA VIDEO SHOOTING ZA NYIMBO YAKE YA CHEKECHA CHEKETUA

Director Meji Alabi akiwa na kijana Ali Kiba washoot video ya chekecha cheletua Nchini Africa kusini. Ni baada ya Ali kiba kukaa kimya kwa muda mrefu kidogo mpaka mashabiki wakidai kuwa anawaangusha ndipo ameamua kuja kwa style hii sasa!

Wednesday, 28 January 2015

Yamoto Band NITAKUPWELEPWETA_Official Video

Hiki ndicho kichupa kipya cha yamoto band. Unaweza kukicheki hapa na kukidownload pia

Wednesday, 14 January 2015

Ali Kiba Atangaza Kuanza Mwaka na 'Surprise'

 Star wa muziki Ali Kiba, amesema kuwa mapokezi ya video yake ya Mwana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania yamekuwa ni ishara kwake kuwa kuna mtu alikuwa amemiss katika game na katika mchango wa kuitangaza nchi kimataifa kupitia sanaa.

Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015
Kiba a.k.a Fundi ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari


Picha na Orodha ya washindi wa tuzo za FIFA Ballon d’Or 2014

cr 2
Tuzo za Ballon d’Or zimefanyika 12 Jan 2014 ambapo wachezaji bora wa mwaka wamepokea tuzo kutoka shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Kupitia Fifa Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi  mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .

Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law  .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
cr 1
ronald

MPYA: DIAMOND AMPA ZARI UJAUZITO #Soma hapa

Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib Abdul – Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa, HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza kudokezwa juu ya ujauzito alionao mwanadada Zari The Boss Lady ambao ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata wapi” ambao wachunguzi wa mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake maarufu wa zamani.

 USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema I can not wait to have you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku akiambatanisha na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye akapost picha yake akichukuliwa vipimo hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha wananchi wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu

Wimbo Wa Daimond mpya January 2015 ‘Nasema Nawee’

DSC_0114

PICHA ZA MAREHEMU ALIYEZIKWA NA KIFARANGA CHA KUKU TUMBONI

Kaburi la marehemu Benadetha Steven aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga aliyezikwa na kifaranga cha kuku tumboni na ndugu zake kwa madai kuwa wanaondoa mikosi katika familia.Pichani ni kaburi lake likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana
 Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za  nyayo za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea pengine umechukuliwa

Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na  sanda ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”

Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena
Mkuu wa upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman Taibu(mwenye suti) akiwa kwenye kaburi la marehemu ambapo alisema jeshi la polisi halina mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali mahakama pekee ndiyo yenye yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi kufukuliwa hivyo kuwaomba wananchi kufukia kaburi hilo badala ya kulifukua.
Benadetha Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu.