Wednesday, 14 January 2015

PICHA ZA MAREHEMU ALIYEZIKWA NA KIFARANGA CHA KUKU TUMBONI

Kaburi la marehemu Benadetha Steven aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga aliyezikwa na kifaranga cha kuku tumboni na ndugu zake kwa madai kuwa wanaondoa mikosi katika familia.Pichani ni kaburi lake likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana
 Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za  nyayo za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea pengine umechukuliwa

Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na  sanda ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”

Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena
Mkuu wa upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman Taibu(mwenye suti) akiwa kwenye kaburi la marehemu ambapo alisema jeshi la polisi halina mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali mahakama pekee ndiyo yenye yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi kufukuliwa hivyo kuwaomba wananchi kufukia kaburi hilo badala ya kulifukua.
Benadetha Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu.

No comments:

Post a Comment