Hiki ndicho kichupa kipya cha yamoto band. Unaweza kukicheki hapa na kukidownload pia
Wednesday, 28 January 2015
Wednesday, 14 January 2015
Ali Kiba Atangaza Kuanza Mwaka na 'Surprise'
Star wa muziki Ali Kiba, amesema kuwa mapokezi ya video yake ya Mwana
ndani na nje ya mipaka ya Tanzania yamekuwa ni ishara kwake kuwa kuna
mtu alikuwa amemiss katika game na katika mchango wa kuitangaza nchi
kimataifa kupitia sanaa.
Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015
Kiba a.k.a Fundi ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari
Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015
Kiba a.k.a Fundi ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari
Picha na Orodha ya washindi wa tuzo za FIFA Ballon d’Or 2014
Tuzo za Ballon d’Or zimefanyika 12 Jan 2014 ambapo wachezaji bora wa
mwaka wamepokea tuzo kutoka shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Kupitia Fifa Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .
Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .
Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
MPYA: DIAMOND AMPA ZARI UJAUZITO #Soma hapa
Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib Abdul –
Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies
aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa,
HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza kudokezwa
juu ya ujauzito alionao mwanadada Zari The Boss Lady ambao
ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata wapi”
ambao wachunguzi wa mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake
maarufu wa zamani.
USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema “I can not wait to have you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku
akiambatanisha na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui
Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye akapost picha
yake akichukuliwa vipimo hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha
wananchi wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika
zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu
PICHA ZA MAREHEMU ALIYEZIKWA NA KIFARANGA CHA KUKU TUMBONI
Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za nyayo
za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika
kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi
wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea pengine umechukuliwa
Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na sanda
ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na
binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa
kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi
hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”
Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena |
Uhusiano wao umeisha 2014, Safaree kayaongea haya mengine kuhusu Nick Minaj…
Mashabiki hupenda kujua kila kinachoendelea kati ya mastaa ambao wana uhusiano wa kimapenzi, Nick Minaj na Safaree hawakuumaliza vizuri mwaka 2014, uhusiano wao uliisha baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10.
Kila mtu alizungumza chake kuhusu wawili hao, Nick aliwahi kusema kuwa hakuwahi kuwa na wakati mgumu katika maisha yake kama wakati ambao aliachana na mpenzi wake huyo.
Safaree Samuels ameonekana
alikuwa na mengi ya kuzungumza juu ya kilichotokea kati yao, kwenye
show ya Power 105 Breakfast Club jamaa amesema kuwa sio kwamba alikuwa
mwanaume muhimu kwa star huyo bali alikuwa ni kila kitu kwake.
Safaree amekiri kuwa yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuamua kuvunja uhusiano huo baada ya kujihisi kuwa amekuwa akitumikishwa na Nick kama mfanyakazi wake na sio mpenzi, alijitahidi kukaa kimya kwa kuwa hakutaka kumharibia staa huyo kwenye kazi yake.
Jamaa amesema kuwa aliuvujisha siri za uhusiano mapya ya Nicki Minaj na Rappa Meek Mill, ambaye aliamua kuwa nae , na kusema hivyo ndivyo ilivyo.
Friday, 9 January 2015
Picha, Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Shirikisho la Soka Afrika,#CAF
Mchezaji wa Man City Yaya Toure ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF iliyokuwa ikiwaniwa na mlinda mlango Vincent Enyeama, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon,
Imekuwa mara ya nne mshambuliaji huyu wa Ivory Coast na Manchester City kushinda tuzo hii kwa mfululizo.
Tuzo hii ilitegemewa kwa asilimia kubwa kushindwa na mlinda mlango kutoka Nigeria Vincent Enyeama.
Thursday, 8 January 2015
Fahamu shirikka bora la usafiri wa anga duniani.
Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika la ndege la taifa la Falme za kairabu United Arab Emirates limetajwa kuwa na ndege salama kuliko zote duniani .
Kwa mujibu wa mtandao maalum unaotoa tathmini ya usafiri wa anga wa www.AirlineRatings.com umeichagua ndege hii kuwa moja ya ndege salama kuliko zote ulimwenguni kwa mwaka 2015 kati ya ndege 449 ambazo zimefanyiwa tathmini duniani kote ambapo jumla ya ndege 149 kati ya hizo zimepewa hadhi ya nyota 7 kama ndege bora katika huduma na usalama.
Mfumo wa kutathmini usafiri wa anga unazingatia vigezo kadhaa ambavyo hutolewa kwa mamlaka rasmi za usafiri wa anga pamoja na taarifa za mashirika ya ndege
Rais wa Etihad Airways ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo James Hogan amesema kuwa siku zote shirika lake limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa usalama na huduma bora vipanewa kipaumbele na watahakikisha kuwa wanaendelea kubaki kwenye nafasi waliyopewa na mtandao huo wa thathmini za usafiri wa anga.
Kampuni ya Etihad Airways ina kituo chake huko Abu Dhabi ambako kuna chuo cha mafunzo ya urubani na nafasi zingine kwenye tasnia ya usafiri wa anga pamoja na wakandarasi wa ndege na pia sehemu hiyo ina karakana kubwa ambako ndege za Etihad hutengenezwa
Mhariri wa mtandao ambao umetoa tathmini Geoffrey Thomas ameisifu Etihad Airlines akisema kuwa kampuni hii ni mojawpao kwenye kundi dogo la makampuni ya usafiri wa anga ambayo yana ubora kuanzia kwenye huduma mpaka kwenye bidhaa
Zimetolewa tuzo za Golikipa bora 10 bora duniani – De Gea ashangaza wengi
Wakati tukisubiri tuzo za mwanasoka bora wa dunia ambaye anategemewa kutangazwa wiki ijayo, shirikisho la historia ya soka na takwimu (IFFHS) limetangaza listi ya magolikipa bora 10 wa mwaka uliopita.
Katika hali ya kushangaza kabisa mchezaji bora wa klabu ya Manchester United msimu uliopita na msimu huu unaoendelea – golikipa kinda wa kihispaniola David De Gea hayumo kwenye orodha hiyo – jambo ambalo limeleta mjadala mkubwa miongoni mwa wadau michezo duniani.
Golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer kwa mara nyingine ametajwa kushika nafasiya kwanza kama golikipa bora duniani.
Kwa mujibu wa takwimu za IFFHS, Neuer ameshinda kwa wastani mkubwa, akiwa na pointi 216 huku anayemfuatia golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois akiwa na pointi 96.
Baada ya kuwa na wakati mzuri kwenye michuano ya kombe la dunia magolikipa kama Keylor Navas na Claudio Bravo nao wameingia kwenye listi hiyo.
Magolikipa wengine waliopo kwenye listi hiyo ni Buffon, Sergio Romero, Ochoa wa Mexico, Hugo Lloris na mwafrika Vincent Enyeama kutoka Nigeria.
Kutokuwemo kwa De Gea, Iker Casillas ambaye ni mshindi wa ubingwa wa ulaya, Copa Del Rey na klabu bingwa ya dunia kumeleta malalamiko mengi.
Monday, 5 January 2015
Mrembo, Blogger na Mfanyabishara Jestina George ameingia deal na Yamoto band ya Kufanya show ya Music Jijini London
Mrembo, Blogger na Mfanyabishata Jestina
George ameingia deal na Yamoto band ya Kufanya show ya Music Jijini
London Mwezi wa Pili Tarehe 21, 2015.
Jestina George Ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:
"Confirmed...21 Feb 2015..Yamoto! Yamoto! Yamoto Band Live in the UK For the first Time Ever...When we Say Live, we mean
Live with Full Band & Dancers. This is one show that's not to be Missed... Sponsored by @officialjestinageorgeblog @bongodeejays@zuriihouseofbeauty
It's gonna be bigger and better! UK & Europe people Save the Date. Their Live Performance is a must see..If you love live music
Make sure you get your tickets mapemaaaa...Hili ni Bonge la show kuwahi kutokea na watoto wameahidi kuweka historia"
Jestina George Ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:
"Confirmed...21 Feb 2015..Yamoto! Yamoto! Yamoto Band Live in the UK For the first Time Ever...When we Say Live, we mean
Live with Full Band & Dancers. This is one show that's not to be Missed... Sponsored by @officialjestinageorgeblog @bongodeejays@zuriihouseofbeauty
It's gonna be bigger and better! UK & Europe people Save the Date. Their Live Performance is a must see..If you love live music
Make sure you get your tickets mapemaaaa...Hili ni Bonge la show kuwahi kutokea na watoto wameahidi kuweka historia"
AFRICA YAZIDI KUMTAMBUA ZAIDI DIAMOND_HUU NI MCHONGO MWINGINE ALIUPATA MSANII HUYU
Diamond Platnumz ateuliwa kutumbuiza CAF
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014.
Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria.
Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo. ..... What more can i say kwa huyu kijana... Go go represent us....
#WhereistheKing????
NANI MZURI ZAIDI KATI YA WEMA SEPETU NA ZARI ZE BOSS LADY??
Kwenye Mitandao ya Jamii Hasa Instagram
kwa Sasa zimeibuka Team Mbili Kubwa zinazoshinda huko kwa Kupeana
Vijembe vya Hapa na Pale Kuhusu Wema Sepetu na Mrembo Zari The Lady Boss
wa Uganda, Ushandani huo wa Team Zari na Team Wema Umekuja Baada ya
Mwanamuziki Diamond Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Wote hao wawili
kwa Muda tofauti ambapo kwa sasa Diamond Ameweka Wazi Kuwa anatoka na
Zari ...
Ubishi mmoja wapo ni kuwa nani ni mzuri wa Umbo na Sura kati ya wema Spetu na Zari , Nasisi hatuna hiyana tumeona tuwabambanishe Hapa tuone nani atapata kura nyingi ...
Haya Nani Mrembo zaidi kati ya Wema Sepetu na Zari The Lady Boss?
Ubishi mmoja wapo ni kuwa nani ni mzuri wa Umbo na Sura kati ya wema Spetu na Zari , Nasisi hatuna hiyana tumeona tuwabambanishe Hapa tuone nani atapata kura nyingi ...
Haya Nani Mrembo zaidi kati ya Wema Sepetu na Zari The Lady Boss?
RIHANNA AANZA KAZI PUMA KWA KUPOST PICHA AKIWA NA CHUPI YA PUMA NA KIFUA WAZI
Mwanamuziki Rihanna Ameanza kazi yake Kwa kishindo aliyepewa na Kampuni ya Mavazi na Viatu vya Puma kama Mkuu wa ubunifu..
Amepost kwenye profile yake picha akiwa amevaa chupi za Puma , Haya wadada kazi Kwenu
"Rihanna who is now the creative director of Puma is sure taking her job seriously. The seductive star showed off her figure in nothing but Puma briefs...
Now every lady would want to rock these"
Amepost kwenye profile yake picha akiwa amevaa chupi za Puma , Haya wadada kazi Kwenu
"Rihanna who is now the creative director of Puma is sure taking her job seriously. The seductive star showed off her figure in nothing but Puma briefs...
Now every lady would want to rock these"
PICHA ZA WOLPER AKIFANYA MAZOEZI ZAWA GUMZO MTANDAONI
Picha za mrembo na mwigizaji wa sinema za kibongo, Jackline Masawe ‘Wolper’ alizoziweka mtandaono akiwa nafanya mazoezi ya viungo zimezua mjadala na maswali mengi.
Wolper ambae kwasaa anaonekana kuwa ‘Bonge’ , wiki iliyopita alitangaza kuanza kufanya mazoezi ili aurudie mwili wake wazamani, toka juzi amekuwa akitupia mtandaoni picha hizo hapo juu akiwa mazoezini.
Mbali na mashabiki wake wengi kumpamoyo kuwa aendelee kukomaa na mazoezi, wapo ambao waliona kama mwanadada japokuwani kweli anafanya mazoezi lakini lengo lake lingine ni kuonyesha watu tattoo zake alizojichora.
Jionee mwenyewe picha hizo, kisha toa mtazamo wako wewe umezionaje?
DeeAndy: Uhusiano wangu na Godzilla una miaka 2 sasa
Hawakuwahi kusema hadharani kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi, lakini wengi walikuwa wakiona ukaribu wa kimahaba uliopo kati ya rapper wa ‘Sala Sala’ Godzilla na mtangazaji wa Clouds FM, DeeAndy. Mtangazaji huyo wa 255 ambayo ni sehemu ya kipindi cha XXL, amelazimika kuthibitisha uhusiano wake na rapper huyo anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa Jumatatu hii.
Good news!! Haya ndio mabadiliko aliyoyaahidi Producer Lamar kwenye muziki mwaka 2015
Producer Lamar baada ya kuanzisha style ya Refix ili kuzipa ngoma za kibongo mzuka zaidi wa kuchezeka na kuleta ladha nyingine masikioni, kwa mwaka 2015 atakuja kitofauti ambapo ataanza kumpatia msanii mdundo (beat) na kurekodi kama Original Song.
Mmiliki huyo wa studio ya Fishcrab alisema; “Well sasa hivi tunaanza kufanya sio Refix tena tunarekodi Original song lakini inakuwa kwenye mdundo ule ule kwa hiyo nitakuwa nagawa mdundo (beat) kwa artist halafu wanafanya wimbo kutokana na mdundo wangu na sio kuchukua acapella zao na kuzi refix pia kutakuwa na events nafanya na dj mwenyewe kwenye Clubs, Beach events“– Lamar.
Nitakuwa nafanya nyingi sana… soon tu nitaanza, sasa hivi nakamilisha sponsors nategemea support nyingi kutoka kwa mashabiki na deals ambazo nimeanza kupata ni kama hizo ku-dj kwenye events na pia tukianza kufanya na Original Song tutafanya na music video tunashoot kabisa“– Lamar.
AY akanusha kuwa na mahusiano na Sitti Mtemvu na Victoria Kimani, asema kwa sasa yuko single
Miongoni mwa watu maarufu wa Bongo ambao huwa hawapendi kuweka hadharani mahusiano yao ya kimapenzi ni pamoja na Ambwene Yessaya a.k.a AY. Baada ya kumuweka hadharani mchumba mpenzi wake 2013, AY amesema kwa sasa yupo single tena. AY na aliyekuwa mchumba mwenye mchanganyiko wa Yemeni na Shelisheli, kwenye Red Carpet ya Road to CHOAMVA 2013
David Moyes Azungumzia Ushindi dhidi Ya Barcelona Na Jina Alilopewa Baada.
David Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Real Sociedad amesema “Kushinda dhidi ya Barcelona ni jambo ambalo aliwaza kwa muda mrefu bila kujua atalifanikisha vipi na hatakama itawezekana “
Kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona, Moyes ambaye alikuwa
manager wa Manchester United alifanikiwa kushinda kwa bao moja bila.Moyes alisema “Ushindi huu umemkumbusha wakati alivyokuwa manager wa Everton, wakati anashinda dhidi ya timu kubwa kama Arsenal, Liverpool na Man United ” yMoes alifukuzwa man utd baada ya miezi kumi kwenye nafasi ya Sir Alex Ferguson.
Mtangazaji maarufu wa soka kutoka Span amembatiza David Moyes jina la ‘Braveheart‘.
Sunday, 4 January 2015
Selena Gomez hana habari na Justin Bieber tena…ala ‘Goodtime’ na mwanaume mwingine Dubai
Selana Gomez amekua Busy na watu wake wa karibu ikiwemo familia yake wakati wa sikukuu za Krismas na mwaka mpya, ili mradi tu aweze kumsahau mpenzi wake Justin Bieber ingawa bado moyo wake unaonyesha dhati kumpenda.
Katika ziara yake Dubai Selana ameonekana kuwa karibu na mwanaume mmoja kwa jina la Harith Bukhash na kuspend naye muda mwingi huku akionyesha dhahiri kumsahaulisha machungu ya kuachana na mpenzi wake Bieber
Mwanaume huyo alionyesha ukaribu zaidi kwa Selena na kumfanya wakati wote kuwa na furaha iliyoonyesha ni jinsi gani anatakiwa kufanyiwa kama malkia.
“Alikua na wakati mzuri sana Dubai na alikua karibu sana na Harith, imeonyesha Selana ni jinsi gani anatakiwa kufanyiwa kama malkia,chanzo cha habari kilieleza.
Yanga yashinda tena kwenye kombe la Mapinduzi.
Washindi wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu uliopita Dar-es-salaam Young Africans Yanga jioni hii wamepata ushindi wao wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar.
Huku wakiwa kwenye kiwango chao bora Yanga walifanikiwa kushinda mchezo wa pili kwa idadi ya mabao manne dhidi ya timu ya Polisi Fc na kufikisha idadi ya mabao nane katika michezo miwili matokeo ambayo yameifanya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali .
Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua dakika karibu 25 kabla ya kuanzidka bao lao la kwanza mfungaji akiwa kiungo wa Kibrazil Andriy Coutinho ambaye alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya mpira kurushwa toka pembeni ya uwanja na kumzidi uwezo beki na nahodha wa Polisi .
Yanga ilifunga bao la pili kwneye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji raia wa Liberia Kper Sherman ambaye alifunga kwa shuti la chini baada ya kupewa pasi ya kichwa na Amisi Tambwe ambaye aliunganisha mpira mrefu uliopigwa na Simon Msuva .
Bao la tatu kwenye mchezo huo kwa Yanga lilifungwa baada ya Andriy Coutinho kupiga mpira wa adhabu ndogo ukitokea pembeni ya uwanja ambapo alipiga mpira huo kwa unfundi mkubwa ukimzidi ujanja kipa wa Polisi .
Bao la nne kwenye mchezo huo lilifungwa na winga Simon Msuva aliyemaliza mpira wa krosi toka pembeni mwa uwanja .
Bao la Msuva lilimfanya aweze kufikisha idadi ya mabao manne inayomfanya we mfungaji anayeongoza katika mashindano haya .
Katika mchezo uliopigwa hapo awali timu toka Uganda KCCA iliwafunga Mtende Fc ya Zanzibar kwa matokeo ya 3-0 .
Fahamu kinachoisibu ndoa ya Kim Kadarshian na Kanye West.
Ndoa ya mastar wawili kwenye anga la Holywood nchini Marekani Kanye West na Kim Kadarshia imeripotiwa kuwa hatarini kutokana na kile kinaotajwa kuwa hali ya kutotimiza majukumu ya ndoa kwa Kanye West .
Watu wa karibu na familia ya wawili hao wameripoti kuwa Kim Kadarshian siku za hivi karibuni amekuwa hana raha kutokana na Yeezy kupoteza hamu ya kuwa naye karibu kutokana na kuwa ‘busy’ na kazi zake za kimuziki na masuala mengine .
Mbaya zaidi ni kwamba Kanye West amekuwa mgumu kumpa Kim haki yake kama mke katika ndoa haki ya ‘unyumba’ kitendo ambacho kimekuwa kimchanganya mrembo huyo na kumfanya akose raha katika ndoa yake changa .
West amekuwa na tabia ya kutofanya mapenzi ya mkewe kwani mara anaporudi nyumbani hutumia muda mwingi kupumzika kitandani au kucheza na mtoto wao North West badala ya kuwa karibu na Kim Kadarshian .
Kwa mujibu wa mitandao ya habari za udaku ikiwemo TMZ na The National Enquirer , Kim Kadarshian amemtaka mume wake kuhudhuria darasa maalum la ushauri nasaha kwa wanandoa ili kuweza kurudisha uhusiano wao katika mstari kabla hali haijawa mbaya zaidi na kusababisha kuvunjika kwa ndoa yao .
Friday, 2 January 2015
Hiki ndicho alichokiandika msanii wa Hip Hop baada ya kutangaza kuacha muziki
Rapper aliyekua akiwakilisha kundi la Lunduno Nikki Mbishi ‘Baba Malcom’ leo ameingia kwenye headline baada ya kutangaza kuwa ameacha kazi ya muziki.
Taarifa hizo aliwahabarisha mashabiki wake kupitia ukurasa wa twitter na kuandika ‘I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry. #2015
Pia ameachia baadhi ya tweets ambazo zimethibitisha msanii huyo kuacha rasmi muziki.
Jamaa huyu kaamua kumlipua mkewe kwa petrol baada ya kukosa chakula cha moto
Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika baadhi ya nchi hususani Afrika.
Huko Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto.
Mwanaume huyo kwa jina la Peter Muthii aliamua kummwagia mkewe mafuta ya petrol akiwa amelala na kumwashia moto na kumfungia ndani kabla ya majirani kuja kumwokoa na kumkimbiza hospitali.
Kisa cha tukio hilo ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimtaka kufanya mwenyewe kitendo kilichomkwaza na kuamua kumlipua kwa kutumia petrol iliyokua chini ya kitanda chao.
Thursday, 1 January 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)