Wednesday, 14 January 2015

Uhusiano wao umeisha 2014, Safaree kayaongea haya mengine kuhusu Nick Minaj…

EQ7xFjRK2n91Aww4OX3DpVCONFuO9pBAWwLf4Kgvnicki-minaj-safaree-samuels-denim-lax-arrival-02 
 Mashabiki hupenda kujua kila kinachoendelea kati ya mastaa ambao wana uhusiano wa kimapenzi, Nick Minaj na Safaree hawakuumaliza vizuri mwaka 2014, uhusiano wao uliisha baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10.
Kila mtu alizungumza chake kuhusu wawili hao, Nick aliwahi kusema kuwa hakuwahi kuwa na wakati mgumu katika maisha yake kama wakati ambao aliachana na mpenzi wake huyo.
Safaree Samuels ameonekana alikuwa na mengi ya kuzungumza juu ya kilichotokea kati yao, kwenye show ya Power 105 Breakfast Club jamaa amesema kuwa sio kwamba alikuwa mwanaume muhimu kwa star huyo bali alikuwa ni kila kitu kwake.
Safaree amekiri kuwa yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuamua kuvunja uhusiano huo baada ya kujihisi kuwa amekuwa akitumikishwa na Nick kama mfanyakazi wake na sio mpenzi, alijitahidi kukaa kimya kwa kuwa hakutaka kumharibia staa huyo kwenye kazi yake.
Jamaa amesema kuwa aliuvujisha siri za uhusiano mapya ya Nicki Minaj na Rappa Meek Mill, ambaye aliamua kuwa nae , na kusema hivyo ndivyo ilivyo.

safaree-samuel-550x345
Safaree Samuels akihojiwa na kituo cha Power 105’s -Breakfast Club

No comments:

Post a Comment