Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika baadhi ya nchi hususani Afrika.
Huko Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto.
Mwanaume huyo kwa jina la Peter Muthii aliamua kummwagia mkewe mafuta ya petrol akiwa amelala na kumwashia moto na kumfungia ndani kabla ya majirani kuja kumwokoa na kumkimbiza hospitali.
Kisa cha tukio hilo ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimtaka kufanya mwenyewe kitendo kilichomkwaza na kuamua kumlipua kwa kutumia petrol iliyokua chini ya kitanda chao.
No comments:
Post a Comment