Monday, 5 January 2015

Good news!! Haya ndio mabadiliko aliyoyaahidi Producer Lamar kwenye muziki mwaka 2015

Producer Lamar baada ya kuanzisha style ya Refix ili kuzipa ngoma za kibongo mzuka zaidi wa kuchezeka na kuleta ladha nyingine masikioni, kwa mwaka 2015 atakuja kitofauti ambapo ataanza kumpatia msanii mdundo (beat) na kurekodi kama Original Song. Mmiliki huyo wa studio ya Fishcrab alisema; “Well sasa hivi tunaanza kufanya sio Refix tena tunarekodi Original song lakini inakuwa kwenye mdundo ule ule kwa hiyo nitakuwa nagawa mdundo (beat) kwa artist halafu wanafanya wimbo kutokana na mdundo wangu na sio kuchukua acapella zao na kuzi refix pia kutakuwa na events nafanya na dj mwenyewe kwenye Clubs, Beach events“– Lamar. Nitakuwa nafanya nyingi sana… soon tu nitaanza, sasa hivi nakamilisha sponsors nategemea support nyingi kutoka kwa mashabiki na deals ambazo nimeanza kupata ni kama hizo ku-dj kwenye events na pia tukianza kufanya na Original Song tutafanya na music video tunashoot kabisa“– Lamar.

No comments:

Post a Comment