Star wa muziki wa r&b Usher Raymond ameamua kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake ambaye amekuwa naye hivi karibuni .
Picha kadhaa za udaku zimemwonyesha Usher akiwa na mpenzi wake huyo anayefahamika kwa jina la Grace Miguel huku mwanamama huyo akiwa amevalia pete ambayo watu wengi wanadhani ni pete ya uchumba .
Mara ya mwisho Usher alikuwa na uhusiano na Tameka Raymond lakini uhusiano huo haukuweza kudumu kwani wawili hao walivunja ndoa yao kwa kutalikiana mahakamani.
Usher kwa muda sasa amekuwa na uhusiano na Grace Miguel ambaye pia Meneja wake na inasemekana kuwa wawili hao watafunga ndoa hivi karibuni .
No comments:
Post a Comment