Sunday, 4 January 2015
Yanga yashinda tena kwenye kombe la Mapinduzi.
Washindi wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu uliopita Dar-es-salaam Young Africans Yanga jioni hii wamepata ushindi wao wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar.
Huku wakiwa kwenye kiwango chao bora Yanga walifanikiwa kushinda mchezo wa pili kwa idadi ya mabao manne dhidi ya timu ya Polisi Fc na kufikisha idadi ya mabao nane katika michezo miwili matokeo ambayo yameifanya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali .
Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua dakika karibu 25 kabla ya kuanzidka bao lao la kwanza mfungaji akiwa kiungo wa Kibrazil Andriy Coutinho ambaye alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya mpira kurushwa toka pembeni ya uwanja na kumzidi uwezo beki na nahodha wa Polisi .
Yanga ilifunga bao la pili kwneye mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji raia wa Liberia Kper Sherman ambaye alifunga kwa shuti la chini baada ya kupewa pasi ya kichwa na Amisi Tambwe ambaye aliunganisha mpira mrefu uliopigwa na Simon Msuva .
Bao la tatu kwenye mchezo huo kwa Yanga lilifungwa baada ya Andriy Coutinho kupiga mpira wa adhabu ndogo ukitokea pembeni ya uwanja ambapo alipiga mpira huo kwa unfundi mkubwa ukimzidi ujanja kipa wa Polisi .
Bao la nne kwenye mchezo huo lilifungwa na winga Simon Msuva aliyemaliza mpira wa krosi toka pembeni mwa uwanja .
Bao la Msuva lilimfanya aweze kufikisha idadi ya mabao manne inayomfanya we mfungaji anayeongoza katika mashindano haya .
Katika mchezo uliopigwa hapo awali timu toka Uganda KCCA iliwafunga Mtende Fc ya Zanzibar kwa matokeo ya 3-0 .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment