Hatimaye Alikiba ameamua kuwajibu baadhi ya wapenzi wa muziki
walioikosoa video ya wimbo wa ‘Mwana’ wanaodai kuwa haiendani na kile
kinachoimbwa.
Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Alikiba amesema
alichokifanya alimaanisha hivyo kuleta picha mpya kwenye vichwa vya
watu.
“Utofauti wa video ndio uzuri wake kwa sababu kila mtu kwenye mind
yake amejenga video, ame-create video itakuwa vipi,” amesema. Kwa sababu
nyimbo imeelezea vitu vingi ni pana kama unavyoona na ina vitu vingi
madawa, ma-prostitute, ukabaji, wizi, vitu fulani vingi sana nisingeweza
vyote kuweka katika video kwa sababu kila mtu anamind yake. Kwahiyo
nilivyofanya utofauti nili-concetrate kwenye dancing na kucheza na
feeling za kuimba. Video nyingi zimeshafanyika duniani sio ya kwangu tu,
kwahiyo watu wasishangae vitendo havikuwepo nimemaanisha sio nimefanya
ili tu nitoe video.”
“Ule utofauti uliokuwepo ndo uzuri wa video yenyewe. Professionals
walifanya hiyo video kwa sababu ni production kubwa iko na watu ambao
wali script vile vile kwahiyo tulishauriana na tuka appreciate kufanya
hicho kitu. Dancing style inaitwa Kalila. Choreographer wangu ndio
alifanya hiyo yote kila kitu.”
No comments:
Post a Comment