Thursday, 8 January 2015

Fahamu shirikka bora la usafiri wa anga duniani.

A6-ETG-Etihad-Airways-Boeing-777-300_PlanespottersNet_252294

Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika la ndege la taifa la Falme za kairabu United Arab Emirates limetajwa kuwa na ndege salama kuliko zote duniani .
Kwa mujibu wa mtandao maalum unaotoa tathmini ya usafiri wa anga wa  www.AirlineRatings.com umeichagua ndege hii kuwa moja ya ndege salama kuliko zote ulimwenguni kwa mwaka 2015 kati ya ndege 449 ambazo zimefanyiwa tathmini duniani kote ambapo jumla ya ndege 149 kati ya hizo zimepewa hadhi ya nyota 7 kama ndege bora katika huduma na usalama.
Mfumo wa kutathmini usafiri wa anga unazingatia vigezo kadhaa ambavyo hutolewa kwa mamlaka rasmi za usafiri wa anga pamoja na taarifa za mashirika ya ndege
Rais wa Etihad Airways ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo James Hogan amesema kuwa siku zote shirika lake limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa usalama na huduma bora vipanewa kipaumbele na watahakikisha kuwa wanaendelea kubaki kwenye nafasi waliyopewa na mtandao huo wa thathmini za usafiri wa anga.
Kampuni ya Etihad Airways ina kituo chake huko Abu Dhabi ambako kuna chuo cha mafunzo ya urubani na nafasi zingine kwenye tasnia ya usafiri wa anga pamoja na wakandarasi wa ndege na pia sehemu hiyo ina karakana kubwa ambako ndege za Etihad hutengenezwa
Moja ya sehemu za kifahari ndani ya ndege za Etihad.
Mhariri wa mtandao ambao umetoa tathmini Geoffrey Thomas ameisifu Etihad Airlines akisema kuwa kampuni hii ni mojawpao kwenye kundi dogo la makampuni ya usafiri wa anga ambayo yana ubora kuanzia kwenye huduma mpaka kwenye bidhaa

No comments:

Post a Comment